21 Agosti 2025 - 12:29
Kiongozi wa Mapinduzi Aomboleza Kifo cha Hujjatul-Islam Naeim Abadi

Mheshimiwa Ayatollah Khamenei ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mwanazuoni mpiganiaji, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Gholamali Naeim Abadi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mheshimiwa Ayatollah Khamenei katika ujumbe wake ametuma salamu za rambirambi kwa kuondokewa na mwanazuoni mpiganiaji, mwakilishi wa zamani wa Kiongozi wa Kidini katika mkoa wa Hormozgan na mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Gholamali Naeim Abadi.

Andiko la ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ni kama ifuatavyo:

Bismillahir-Rahmanir-Rahim
Kifo cha mwanazuoni mpiganiaji, Mheshimiwa Hujjatul-Islam Naeim Abadi (Rahmatullah ‘Alayh) nakitumia rambirambi zangu kwa familia tukufu, marafiki na wapenzi wake.

Juhudi kubwa za marehemu huyo na baadhi ya watu wake katika kufundisha na kueneza masuala ya dini ni jambo linalostahili kusifiwa na kupongezwa.
Rehema ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake.

Sayyid Ali Khamenei

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha